Storymoja

Celebrating East African Writing!

Masterclass: Siri ya Kuandika Kazi za Kiubunifu

Masterclass: Siri ya Kuandika Kazi za Kibunifu

With: Ken Walibora

Time: Thursday 19th September 2pm – 5pm

Venue: Nairobi National Museum
 
Ubunifu ni kuona yale ambayo hayapo na kuyafinyanga mpaka yawe kama yapo, kuyafanya yahisiwe, yasikiwe, na muhimu zaidi yaonekane. Tokeo ni kwamba uhalisia wa kibunifu unakuwa umechukua sura ya uhalisia halisi kiasi kwamba
wasomaji watasema haya lazima yalitukia au yalimtukia mwandishi.
 
Ni nini ndiyo siri ya kuandika kazi za kibunifu zenye kuhisika, kusikiwa na kuonekana “kweli” kiasi cha kuaminika kana kwamba ni halisi? Ni nini siri ya kisanii ya kuuangusha ukuta kati ya kweli ya fasihi na kweli ya maisha halisi? Tunawezaje kuwa na wahusika wa kusadikika na kukumbukika, hadithi ya kupigiwa mfano, na mtiririko unaotiririka vizuri na kumpa msomaji raha na buraha pamoja na kina cha fikra?
 
Majibu ya maswali haya na mengine atayatoa Prof. Ken Walibora katika wasilisho lake…

Usikose ujiume kidole!
 
Get an Early Bird Festival Ticket TODAY and enjoy a FREE pre-registered Masterclass. [Early Bird Deal valid only until 30th August!]
 
Register-black

Advertisements

Information

This entry was posted on August 13, 2014 by in Writer's Blog.
%d bloggers like this: