Storymoja

Celebrating East African Writing!

Mwito kwa Waandishi na Wahariri

Tunazitaka hadithi zako. Tunazihitaji hadithi zako. Tunahitaji hadithi za KWETU. Hadithi za kweli, hadithi za kibunilizi, hadithi za kifantasia, zinazobadilisha maisha ya wasomaji, hadithi za kiasili na nyingine nyinginezo. Tunahitaji hadithi kutoka maeneo ya pwani, maeneo ya ziwani, maeneo ya mlimani, maeneo ya Bonde la Ufa, maeneo ya Kaskazini na maeneo mengine yote nchini Kenya. Tutumie hadithi zilizoandikwa kwa Kiingereza na Kiswahili. Tunakuhitaji uandike kwa ajili ya kampeni ya mageuzi itakayolichangamsha na kulihamasisha taifa zima. 

Wewe ni nani? 

 • Mwandishi ama mhariri mwenye ari na msukumo wa ndani kwa ndani kuhusu kusoma na kuendeleza desturi ya usomaji na uandishi nchini Kenya.
 • Mwandishi au mhariri apatikanye kokote nchini Kenya lakini mwenye uzoefu wa kutumia mitandao ya kijamii kila uchao.
 • Mwandishi au mhariri mwenye nia ya kutenga na kutumia angalau saa mbili kwa siku kwa ajili ya kubuni kazi yenye maneno 1,000 kila siku kwa muda wa miezi mitatu.
 • Mwandishi au mhariri atakayepatikana kuhudhuria warsha ya mdukizo itakayofanyika Septemba 19, 2015 kutoka saa kumi alasiri (4pm) hadi saa kumi na mbili unusu jioni (6.30pm).

 

Tunahitaji kusikia maoni yako. Tutumie kitini kifupi chenye maelezo kuhusu:

 • Jina lako na maelezo kuhusu namna ya kuwasiliana nawe.
 • Wasifu wako mfupi na maelezo mafupi kuhusu uzoefu na harakati zako za uandishi.
 • Mabadiliko unayotazamia kuyashuhudia katika desturi ya uandishi na usomaji nchini Kenya.
 • Tutumie sampuli fupi ya kazi yako ya uandishi (idadi ya juu ya maneno ikiwa 500) ama kiungio kitakachotufikisha kwenye kazi yako iliyopo mtandaoni.

Tuandikie kwa: stories@storymojaafrica.co.ke. Siku ya makataa ya uwasilishaji wa kazi ni Jumatano, 16/9/2015, saa kumi na moja kamili za jioni (5.00pm)

Ni nini tunachokuahidi? 

 • Kazi utakayowasilisha kwa ajili ya kampeni hii itaacha athari kubwa chanya nchini Kenya na nje ya mipaka yake.
 • Tutafidia gharama zako za kuandaa kazi na pia tutakulipa mrabaha kwa kazi yako.
 • Tutayashughulikia maswali na maoni yako kwa heshima ipasavyo kwani, mtu ni watu.”

Reading is cool. Kusoma ni Poa!

Information

This entry was posted on September 14, 2015 by in Writer's Blog.
%d bloggers like this: