Storymoja

Celebrating East African Writing!

Mwito Wa Storymoja Wa Kuwasilishwa Miswada Ya Fasihi Bunifu Na Mwaliko Wa Warsha

Mwaliko katika warsha ya uandishi  

MISURURU YA HADITHI KUHUSU STADI ZA MAISHA – hadithi bunifu kwa vijana chipukizi katika Kingereza na Kiswahili 

Tafadhali, tuma ombi la kuhudhuria warsha ikiwa:

1.      Ungependa kuitikia mwito wa kuwasilisha mswada ulioafikia vigezo vilivyotolewa hapa chini lakini mswada wenyewe haujaandikwa au kukamilishwa.

2.      Ikiwa una mswada ambao huna hakika utaafikia vigezo vilivyotolewa na una nia ya kujua jinsi ya kuufanya uafikie maagizo hayo na kuuhariri.

3.      Ikiwa una nia ya kufahamu na kujifunza mbinu za kimsingi za ubunifu (jinsi ya kuwakuza wahusika, dayalojia au semi halisi za wahusika na mandhari ya maonesho/matukio, kujihariria na kuandaa ploti ya hadithi tarajiwa) zitakazokuwezesha kukuza mswada wako bunifu ili kukupa hakikisho takriban kamili kuwa tutachapisha mswada wako.

 

WASIMAMIZI WA WARSHA: Muthoni Garland na Rebecca Nandwa

TAREHE ZA WARSHA (unaombwa kutoa hakikisho la kuhudhuria vikao vyote sita) 

Siku – Jumamosi: Januari 30; Februari 6; Februari 13; Februari 20; Aprili 2 na Aprili 9. 2016.

Saa –  Kuanzia 9:50 asubuhi hadi  1: 00 adhuhuri.

Kiingilio – Shilingi 1,000 kwa kila kikao (Ukihitaji  usaidizi wa kifedha, tuandikie; yaani ukosefu wa pesa usikuzuie kuhudhuria warsha)

Nafasi/Idadi ya nafasi–  Zisizozidi 18

Mahala: Ofisi za Storymoja, Spring Valley, Panda gari nambari 118 kutoka Khoja, Nairobi, shuka Spring Valley Shopping Center, tembea hatua chache hadi Shanzu Road, na uingie Gate no. 2

Ili kutuma ombi lako na kujitengea nafasi, tuma baruapepe na uambatanishe wasifu wako mfupi pamoja na kielelezo cha mswada wako usiozidi maneno 500 kufikia tarehe Januari 25, kwa info@storymojaafrica.co.ke

 

 

MWITO WA UWASILISHAJI WA MISWADA

Storymoja inawaomba waandishi kuwasilisha miswada itakayochapishwa chini ya msururu wetu wa STADI ZA MAISHA kwa mujibu wa vigezo hivi: 

 1. Hadithi lazima iwe na maneno kati ya 30,000 na 80,000 na itumwe kwa baruapepe kupitia info@storymojaafrica.co.ke.
 2. Hadithi inaweza kuwa bunifu au halisia.
 3. Sharti hadithi iafiki umri wa wasomaji lengwa. Wasomaji lengwa waandikwe katika ukurasa wa kwanza chini ya anwani ya hadithi.
 4. Mpangilio – nafasi mbili katikati ya kila sentensi, fonti iwe Calibri, Roman Times au Arial; 12. Lazima uandike anwani, jina la mwandishi, nambari ya ukurasa na tarehe katika kila ukurasa kama header.
 5. Hata ikiwa kazi yako ni bunifu, mandhari yako yawe halisi na yaweze kubainika/kutambulika kwa urahisi. Unashauriwa kuangazia mambo, maudhui, mandhari na kadhalika yaliyomo katika mazingira ya wasomaji wanaolengwa.
 6. Tumia uzungumzi nafsia kwa upana ili msomaji aone safari ya mhusika mwema, mkuu/shujaa katika kujitambua hadi kufaulu kwake/kutofaulu kwake.
 7. Hadithi lazima iandikwe kwa Kingereza au Kiswahili.
 8. Hadithi inaweza kuchukua mkondo wowote wa usimulizi– masimulizi ya moja kwa moja, jazanda, ugunduzi wa mambo, mambo yenye uhalisia, fasihi bunifu ya kisayansi na kadhalika.
 9. Wahusika waaminike/ wawe na uhalisia. Mhusika mkuu mwema lazima ajitokeze kama mkazi halisi wa Afrika Mashariki.
 10. Matukio yadhihirike yenyewe; usiyahubiri/kuyasimulia kwa ufupisho. Matukio yafanyike katika wakati halisi na utumie matendo na dayalojia nyingi kadri inavyowezekana kusimulia hadithi yako –punguza mbinu rejeshi/visengere nyuma na maelezo ya kufupisha matukio. Dayalojia zako zionekane kama maneno halisi yanayozungumzwa na wenyeji wa Afrika Mashariki. Tumia uzungumzi nafsia pia.
 11. Sadfa zinaweza tu kutokea katika ukurasa wa kwanza. Usilete mhusika mpya ambaye ana nafasi kubwa katika kukuza ploti baada ya hadithi kupita katikati/kilele. Epuka wahusika ambao wanajitokeza kimiujiza kutatua mgogoro.
 12. Hadithi iwe na mgogoro mmoja mkuu unaokuza mojawapo wa maudhui yafuatayo:

 

 

 Uhusiano– mvulana/msichana Ushawishi wa rika Kujisimamia
Familia Tabaka katika jamii Afya  – hasa Ukimwi, kisukari, afya ya akili
Mazingira, jamii Ubaguzi kuhusiana na miaka Maadili
Kitambulisho – kabila/rangi ya ngozi/binafsi Mazingira Kubaleghe
Ubaguzi wa jinsia Kujiamini Rasilmali – asilia ama kutengenezwa
Kubuni mali ama kusimamia mali Vielelezo Utamaduni
 1. Katika kushughulikia na kutatua mgogoro katika hadithi, wahusika wakabiliana na baadhi ya mbinu za maisha zilizotajwa hapa chini. Mhusika mkuu hana budi kujifunza ama kutambua umuhimu wa ujuzi tekelezi muafaka katika hadithi. Kwa mfano, ikiwa wamepuuza majukumu, matukio yanayowapata yanastahili kuwasaidia kubadilika na kutekeleza majukumu hayo.
Jukumu    Huruma /Ukarimu /Utunzaji
Kujiamini Hamu ya kujua
Heshima Maisha ya kiroho
Ubunifu/kufikiria. Upembuzi, uchanganuzi,
Uamuzi  Mwelekeo
Kufanya uamuzi /kukabiliana na matokeo ya maamuzi Lenga
Maadili ya kazi Kujiamini
Utatuzi wa changamoto Ujuzi wa utekelezi
Azma Mienendo
Ustahamilivu/umakinifu Utumiaji bora wa muda
Matumizi ya pesa Mapenzi yenye manufaa, yasiyo na manufaa
Uzalendo Uhuru
Mawasiliano Jitihada, adili
Msukumo/ari/hamu Kusikiza
Ucheshi/uwezo wa kujicheka Uongofu
Kukabiliana na hisia/mabadiliko ya hisia Kujitambua/Kujiamini/Kujitathmini, upevu ama ukomavu wa hisia
 1. Mhusika mkuu (shujaa) katika hadithi:
 2. Lazima awe kati ya miaka 13 na 18
 3. Lazima awe na ari ya kutaka kitu ama jambo kufanyika
 4. Lazima achukue hatua, asukume matukio kutendeka katika hadithi (siyo kila wakati wote mambo yamkumbe).
 5. Lazima ateseke (kihisia) na kimazingira kwa sababu ya hatua hizo.
 6. Lazima awe mhusika mkuu anayesuluhisha mgogoro huo.
 7. Hana budi kuishi!
 8. Lazima awe na mabadiliko; ajifunze kutokana na matukio ya hadithi.
 9. Lazima kila sura iishie katika hali ya taharuki-iwe ndogo ama kubwa.
 10. Mafunzo ya ujuzi tekelezi hayana budi kuonekana msomaji anapotamatisha kusoma hadithi. Jiepushe na kueleza ‘adili’ ama ‘ujuzi tekelezi’ wa hadithi. Ionyeshe katika hadithi na kumpa msomaji fursa ya kujitafsiria ujuzi wenyewe.
 11. Kuwa huru kutumia vichekesho,mzaha, unavyotaka (kwa mfano jamii inayokabiliana na uvamizi wa nzige ama ama kijana anayekabiliana na chunusi anapokutana na mpenzi wa kike)
 12. Onyesha ubunifu!

.

 

UCHAPISHAJI

Punde to Storymoja inakubali kirasmi kuchapisha mswada, tutauhariri, kuupa kichwa, kusoma, kuruwaza, kuchapisha, kutangaza na kusambaza kazi tukisimamia gharama zote kuambatana na utaratibu wetu.

Tutashirikiana pakubwa na mwandishi na kutarajia mwandishi kujitolea zaidI hasa wakati wa uhariri na utangazaji wa kitabu. Tunataka wandishi kufanikiwa.

 

MALIPO

 1. Lazima mwandishi aweke sahihi katika mkataba wa kuthibitisha yeye mwenyewe aliandika miswada na haijachapishwa kwingine.

 

 1. Mwandishi atachagua ikiwa:
 • Atakubali malipo ya jumla ya shilingi moja kwa kila neon, kuambatana na hesabu ya mwisho ya maneno baada ya uhariri, kwa haki zote duniani na katika hali yoyote, nakala za mwisho zinapowekwa sahihi; ama
 • Akubali malipo ya mrabaha ya asilimia 10 kwa mauzo, kwa haki zote duniani na katika hali zote, zinazojumuishwa mara mbili kila mwaka na kulipwa kila mwaka.

 

ANZA KUANDIKA SASA!

 

Advertisements
%d bloggers like this: